Hivyo pamoja na mkakati wa John Shabani wa kujitolea kuwatembelea watu wanaoishi katika mazingira magumu na kutafuta namna ya kuwasaidia, mwanaharakati wa kujtolea wa haki za binadumu John Shabani; safari hii ameungana na mwanamama mwenye uchungu wa kutetea haki za mjane Bi Rose Sarwatt na kuanzisha chama cha wajane Tanzania.
Chama cha Wajane Tanzania (Tanzania Widows Association)
chenye usajili na S.A. 19708, ni chama kilichoanzishwa
rasmi mnamo mwaka 2014, kikiwa na lengo la kuwaweka wajane pamoja, ili
kutambuana, kufahamiana, kujua changamoto mbalimbali anazopitia mjane, na
kutafuta ufumbuzi wa kutatua changamoto hizo.
Ikiwemo kusomesha watoto, elimu ya sheria, afya, saikologia, biashara na
ujasiriamali.
Vilevile chama
kinajihusisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya mjane, iwatambue wajane,
kuwapenda, kuwathamini na kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine, pia kujitoa
kwa hali na mali kusaidia kupambana na changamoto anazopitia mjane. Pia chama kinasimamia sheria inayotetea haki
za mjane Tanzania, ikiwemo hati ya mirathi na usimamizi wa mali za familia
baada ya kifo cha mume wa mjane. Hivyo chama
hiki kitarejesha matumaini mapya kwa mjane, na wajane watarajiwa. Pia kwa namna moja au nyingine, kujihusiha na
haki za mgane na watoto walioachwa na wazazi (yatima).
Mawasiliano
CHAMA CHA WAJANE TANZANIA
“Tanzania Widows Association”
“Tanzania Widows Association”
P.O.Box 33476,
Dar es salaam
Simu:
+255 754 366 530 – Mwenyekiti
+255 713 778 778 – Katibu
E-mail: widowstz@gmail.com
FACEBOOK: Widows Tanzania
TWITTER: @TanzaniaWidows
0 comments:
Post a Comment