Nasema asante kwa MAKAO YA KULEA WATOTO YATIMA ( CHAKUWAMA)
Nimejisikia raha kuwahudumia, tumekuwa na wakati mzuri wa kula na kunywa pamoja.
Lakini pia nimshukuru Mtumishi wa Mungu Mgisa Mtebe kwa kushiriki lakini pia kutoa ujumbe maalum katika tukio hilo. Mwisho pongezi za pekee zimwendee rafiki yangu Edson mhasisi wa "WORLD DOMINION INTERNATIONAL MINISTRIES" kutoka South Africa kwa kujitoa pamoja na marafiki wote mliohudhuri tukio hili la chakula cha upendo.
Mathayo 7:12
Unapokuwa na afya, unapokuwa na uzima, unapokula na kulala vizuri, unapopanga bajeti ya kuwapeleka watoto international schools, unapofanikiwa, kumbuka wapo wengine katika jamii hawana hata matumaini ya kesho, kumbuka wapo yatima, wajane, wazee na watu wenye ulemavu wanaotuitaji. Tuwatembelee, tuwasaidie.
0 comments:
Post a Comment