Saturday 17 November 2018

KWA WAZAZI/WALEZI NA WAZAZI WATARAJIWA ZINGATIA HAYA MAMBO 10 MUHIMU KWA MALEZI BORA YA MTOTO

 1.Mkanye Mtoto Wako wa Kike Hata Wakiume,Kuusu Kupakatwa Ovyo bila Kujali ni nani Anampakata,Hata Kama Ni Mjomba wake.
2.Usivue Nguo Mbele ya Mwanao Pindi Akifikisha Miaka Miwili Au zaidi,Mwambie Akupishe Uvue Nguo.
3.Usiruhusu Mtu Yeyote Amuite Mwanao"Mchumba,Mke wangu au Mme wangu"
4.Mwanao Akienda Kucheza Akikisha Anacheza nini,Siku Hizi Watoto Wanacheza Michezo Michafu na Watoto wengine Wanamaambukizi.
5.Kama Mwanao Hapendi Kwenda Kwa Mtu Flani Usimlazimishe,Pia chunguza Ujue Sababu.
6.Nakushauri Pitia Muvie Yeyote Kabla Mtoto Kuaangalia ili Uchague Yenye Maadili Mazuri.
7.Mtoto Anapofikisha Umri wa Miaka Mitatu,Anza kumfundisha kusafisha Mwenyewe sehemu zake za Siri,Na Umkataze Kabisa Mtu Kushika Sehemu Hizo.
8.Mfundishe Mtoto Kumcha Mungu na Sio Kufata Mkumbo.
9.Mtoto Akilalamika Kuusu Mtu Flani,Usipuuze Fanya Uchunguzi.
10.Usipende Kumruhusu Mwanao kulala na Housegirl au Houseboy Au mgeni,Baadhi Yao Sio Waaminifu,Huwezi Jua Tabia Za watu na watakachokitenda Usiku.

Comment & Share Tafadhali
Mungu Akupe Familia Bora

#johnshabani

www.singleparentchildren.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment