Monday, 24 June 2019
SJ STUDIO NA MKAKATI WA KUSAIDIA WATOTO WENYE VIPAJI VYA KUIMBA
12:03
No comments
Kipaji Kipaji ni zawadi, ni nguvu ya ndani aliyonayo binadamu, inayomwezesha kufanya shughuli zake katika uhalisia wake, na tena bila kutumia nguvu nyingi (Enearta 2005).
Tuna Mifano mingi ya watu wengi waliofanikiwa Tanzania, Afrika na duniania, si kwasababu wamesoma sana, au wamezaliwa katika familia Tajiri, lakini kwasababu ya vipaji vyao kikiwemo kipaji cha muziki au kuimba. Kuna kuimba kwaajili ya kipaji, kuna kuimba kwa kupata mafunzo (skils) na kwa wakristo kuna kuimba kwa ajili ya upako (anointing)
John Shabani na studio yake amekuwa akijitolea kuibua na kufundisha waimbaji wengi, ili kupitia vipaji vya uimbaji kwanza wamtumikie Mungu kisha iwasaidie kimapata kwamaana ya kuuza kazi zao, lakini pia kuwatengenezea platform ya kukutana na watu mbalimbali. Safari hii tumeamua kujitolea kusaidia watoto wenye vipaji vya kuimba. Mlee mtoto kimaadili, mlee mtoto kiroho, mlee mtoto kielimu lakini pia ni muhimu kumlea mtoto kivipaji.
Kila jumamosi asubui, tunakutana na watoto pale studio, tuna wafanyia majaribio kidogo, tuna wafundisha kisha watakaokuwa vizuri wanarekodiwa nyimbo moja ya kutangazia kipaji. Hivyo mzazi,ndugu,rafiki hujachelewa..Mlete mtoto.
Lakini pia nikushirikishe kuungana nami kusaidia watoto wenye vipaji lakini wanaishi katika mazingira magumu (JOIN ME TO HELP OUR CHILDREN) Haya yamekuwa maisha yangu, kuhakikisha maisha ya watoto wetu hasa yatima na waishio katika mazingira hatarishi/magumu, walio athiriwa kisaikolojia kwa kunyanyaswa, kulawitiwa, kubakwa na kufanyiwa kila aina ya unyanyasaji wa kijinsia wanasaidika.
Nimeyafanya haya siku zangu zote, nimeyafanya haya kwa moyo wangu wote, nimeyafanya kwa kujitolea nikimshirikisha kila mwenye moyo wa kusaidia, nimeyafanya kwa kupitia taasisi na mashirika mbalimbali, nimeyafanya kwasababu namimi nilikulia na kulelewa katika mazingira hayo.
Nimekuwa nikiwafundisha Neno la Mungu ili wajue kumtegemea Mungu, kutokuwa na visasi, kusamehe na kumpenda kila mtu, ninaibua vipaji na kuviendeleza, natafuta namna yoyote ya watoto hao kupata elimu bora, wasio na chakula au mavazi tunatafuta namna ya kuwasaidia.
KARIBU TUSHIRIKIANE