Katika kuendeleza mkakati wa kutetea haki za wanawake, mwanaharakati wa haki za binadamu, John Shabani, akishirikiana na marafiki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, waliamua kumtia moyo mwanamama Lightness Bayo. Bi Lightness Bayo, akmekuwa na mzigo mkubwa wa kuwasaidia wanawake na mabinti waliotelekezwa baada ya kupewa ujauzito
Baada ya kuguswa na mambo anayofanya mama huyo, ikiwa ni pamoja na kuwa na shule ya ufundi, shule ya msingi,mitaji midogo ya kifedha kwa wasionacho, ndipo John alipoamua kujitolea kufanya kusimama na mama huyo.
Kituo kiko wilaya ya karatu mkoa wa Arusha.
Kwa habari zaidi, tuendelee kuwasiliana