Friday, 18 April 2014

LIGHTNES BAYO, MAMA ALIYEJITOLEA KUWAKOMBOA MABINTI WANAOZALISHWA KATIKA UMRI MDOGO NA KUTELEKEZWA

Kwa wakaaji wa karatu na vitongoji vyake, jina la Lightness Bayo si ngeni masikioni mwao, kwani ni mwana mama alieamua kuyatumia maisha yake katika kuwasaidia mabinti waliozalishwa na kutelekezwa, mabinti hao ni wale hasa wenye umri mdogo. Pamoja na mabinti pia mama huyo amekuwa akiwasaidia watu wenye uhitaji mbalimbali wakiwemo wajane na yatima. Ili kuweza kuwasaidia watu hao Bi Lightness akisaidiana na wafadhili mbalimbali, amejenga kituo cha ufundi “Lake Eyasi Girls Vocation Training Center”,katika kijiji cha Mang,ola wilaya ya karatu.

Kituo hicho kimeweza kuinua kipata cha mabinti waliokuwa hawajiwezi na wengine kutaka kujiua. Moja ya mambo yanayofanyika katika kituo hocho ni kujifunza ushonaji na ufumaji. Pia mama huyo ameweza kuwasaidia jamii ya wamang’ati kwa kuwaanzishia mrati wa kufuga mbuzi na nyuki wa asali. Pamoja na kituo hicho, pia anacho kituo cha kulea watoto yatima.

Hata hivyo shule anayoiongoza yeye na mume wake katika mji wa karatu Tumaini Junior School, ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri nchini.

Inawezekana wewe ni Binti, umezalishwa na kutelekezwa, au unaye binti wa aina hiyo, au ungependa kuwa rafiki wa maono haya ya Bi Lightness, kwa kumuombea, kumtia moyo au kuchangia chochote, basi usisite kuwasiliana naye kwa simu namba 0754317394

        John Shabani katika kijiji cha Mang'ola huko karatu
Bi Lightness akimuonyesha John shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo cha Lake Eyesi Vocation Training Center

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment