Baada ya kuzunguka nchi kadhaa barani Afrika na kujionea hali
ngumu ya maisha ya watu hasa kina mama watoto na vijana, John Shabani yuko
mbioni kukamilisha usajili wa taasisi yake ijulikanayokama HOPE TRUST, yenye
lengo la kutafuta ufumbuzi katika kuwasaidia watoto, kina mama, vijana na wote waishio katika mazingira magumu
Taasisi hiyo itajikita katika kutafuta ufumbuzi katika
kuwasaidia watoto, vijana na kina mama wanaoishi katika mazingira magumu. Hivi
karibuni John alifanya ziara huko Turkana Kenya maali ambapo kuna jamii ya watu
wanaoishi katika mazingira magumu sana na walioshikilia mila na tamaduni zilizo
kinyume na haki za binadamu, pia alitembelea katika moja ya kambi kubwa ya
wakimbizi barani Afrika; kambi hiyo inaitwa KAKUMA, yenye wakimbizi kutoka
Uganda, Rwanda, DRC Kongo, Burundi, Somalia, Rwanda n.k.
Pia John alitembelea vijiji kadhaa huko Sudan, na kujionea
jinsi maisha yalivyo magumu hasa kutokana na vita vya mara kwa mara katika nchi
hiyo amba yo hivi karibuni imegawanyika na kuwa nchi mbili.
Kwa upande wa Tanzania, John amekuwa akifanya ziara
mbalimbali, akitembelea jamii ya watu wanaoishi katika mazingira magumu na hasa
wale waliokumbatia mila zinazorudisha nyuma maendeleo. Katika ya makabila hayo
ni wa Hadzabe, wa Mang’ati, wa Masai na makabila mengine madogomadogo.
Kwa msaada wa Mungu, John amepanga kutembelea huko Somali,
Kongo, Misri na nchi zingine barani Afrika.
Pia ili kuibua vipaji kwa vijana na watoto na kuviendeleza,
ameanzisha kituo cha kuibua vipaji, na kwa kuanza, ameanzisha kituo cha kuibua
vipaji vya uimbaji na uigizaji. Mpaka sasa kituo hicho kimeibua vipaji vya
watoto 35, vijana 105 na watu wazima 22.
Unapoomba, usisahau kulitaja jina la John Shabani, mwana
harakati aliyejitolea kwa nguvu zake, Vipaji vyake pamoja na uwezo wake mdogo
kuwasaidia watu wengine.
Watu hawa wanahitaji msaada wa kila aina ili waweze kuishi
kama mwanadamu mwingine.
Wito wangu, ni kwa kila mtu kuguswa na na hali hii na
kuungana namikatika kuwasaidia ndugu zetu hawa. Usiulize serikali imekufanyia
nini, bali jiulize umechangia nini katika serikali yako. Kumbuka amsaidiaye
maskini humkopesha Mungu, na Mungu wetu hawezikukaa na deni la mtu,yeye hulipa
mara mia. Ukitaka kujua maisha magumu, tembelea vijijini. Kumbuka mchango wako
wa hali na mali ni wa muhimu sana. Mchango wako na wangu hakika unaweza
kuwasaidia ndugu zetu hawa.
0 comments:
Post a Comment